Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Biteko ashiriki ufungaji Maonesho ya Madini Geita


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Oktoba 13, 2024 mkoani Geita ameshiriki katika hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya Saba ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wakati akimkaribisha  Rais Mhe. Dkt. Samia kuhutubia wananchi, Dkt. Biteko amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kuikuza na kuimarisha sekta ya madini nchini.

“ Wachimbaji wakubwa na wadogo wamekuwa wanatembea daraja la juu kwa sababu ya fursa ulizotoa kwao. Nataka niwaambie wananchi wa Geita na Watanzania kwa ujumla kuwa Mhe. Rais amekuwa akifanya kila jitihada kwa kuwa anataka mnufaike na raslimali zilizopo nchini.” Amesema Dkt. Biteko.

=MWISHO=