Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maudhui ya Ndani
Lengo
Kuratibu, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa masuala ya uwezeshaji kiuchumi na ushiriki wa watanzania “Local Content”.
Majukumu ya Idara
Idara itatekeleza majukumu yafuatayo: -
- Kuandaa, kufuatilia, kutathmini na kupitia utekelezaji wa sera, mikakati, programu, sheria na miongozo kuhusu uwezeshaji kiuchumi, na ushiriki wa watanzania;
- Kuratibu utekelezaji wa sera, sheria, kanuni na miongozo kuhusu uwezeshaji kiuchumi na ushiriki wa watanzania;
- Kufuatilia na kutathmini viwango na utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo inayohusu masuala ya uwezeshaji kiuchumi na ushiriki wa wazawa nchini;
- Kukuza na kuimarisha ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati na uwekezaji Inayotekelezwa nchini;
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kuhusu masuala ya uwezeshaji kiuchumi na ushiriki wa watanzania;
- Kuhamasisha masuala ya ushiriki wa watanzania katika Wizara, Taasisi, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuweka mazingira wezeshi ya watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi;
- Kuratibu, kusimamia na kutathmini utendaji wa Mifuko na Programu za Uwezeshaji Kiuchumi katika Wizara za kisekta na sekta binafsi;
- Kukuza manufaa yatokanayo na ushiriki wa makundi maalumu katika ununuzi wa umma ili kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa;
- Kuratibu, kusimamia na kutathmini utendaji wa vituo vya uwezeshaji nchini;
- Kusimamia masuala yote yanayohusu uwezeshaji kiuchumi na ushiriki wa wazawa yanayotekelezwa na sekta binafsi kwa kushirikiana na Wizara za kisekta;
- Kuhamasisha na kuimarisha Majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika ngazi zote kupitia Mabaraza ya Biashara ya Wilaya (DBCs), Mabaraza ya Biashara ya Mikoa (RBCs), Mabaraza ya Majadiliano kati ya Wizara na Sekta Binafsi (MPPD) na Baraza la Taifa la Biashara (TNBC);
- Kuratibu, kusimamia na kutathmini utekelezaji wa maazimio ya mikutano ya mabaraza ya Wilaya (DBCs), Mikoa (RBCs), Wizara (MPPD) na TNBC;
- Kuratibu uwekaji mazingira wezeshi ya uwezeshaji kiuchumi na ushiriki wa wazawa katika Wizara zote za kisekta;
- Kuratibu tafiti kuhusu uwezeshaji kiuchumi na ushiriki wa watanzania, pamoja na na kupendekeza hatua za kuimarisha ukuaji wake;
- Kufuatilia na kutoa mwongozo kuhusu utekelezaji wa masuala ya uwezeshaji kiuchumi na ushiriki wa Watanzania kwenye sekta binafsi; na
- Kusimamia na kufuatilia utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Baraza la Taifa la Biashara (TNBC).
Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi na ina Sehemu Mbili kama ifuatavyo: -
- Uwezeshaji Kiuchumi; and
- Maudhui ya Ndani “Local Content”.
Sehemu ya Uwezeshaji Kiuchumi
Sehemu hii inatekeleza majukumu yafuatayo: -
- Kuandaa na kupitia Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo, mikakati, programu, na miradi kuhusu Uwezeshaji Kiuchumi;
- Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo kuhusu Masuala ya Uwezeshaji Kiuchumi;
- Kufuatilia na kutathmini viwango na utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo kuhusu masuala ya Uwezeshaji Kiuchumi katika Wizara, Miko ana Mamlaka za Serikali za Mitaa;
- Kufanya mapitio ya sera za kisekta kwa lengo la kubaini ufanisi katika kujibu mahitaji ya uwezashaji kiuchumi;
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa sekta ya umma na sekta binafsi kuhusu masuala ya uwezeshaji kiuchumi;
- Kuratibu na kusimamia utendaji wa Mifuko na Programu za Uwezeshaji Kiuchumi zinazoratibiwa na kusimamiwa na Wizara na Taasisi za kisekta na Sekta ya Binafsi;
- Kuratibu, kusimamia na kutathmini utendaji wa Vituo vya Uwezeshaji Kiuchumi;
- Kusimamia masuala yote yanayohusu uwezeshaji kiuchumi yanayotekelezwa na sekta binafsi kwa kushirikiana na Wizara za kisekta;
- Kuratibu Maonesho ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Kiuchumi;
- Kuratibu utoaji wa huduma jumuishi za Uwezeshaji Kiuchumi kwa Wizara na Taasisi za kisekta;
- Kuratibu tafiti na tathmini kuhusu masuala ya Uwezeshaji Kiuchumi pamoja na kupendekeza hatua za kuimarisha ukuaji wake;
- Kufuatilia na kutoa mwongozo kuhusu utekelezaji wa masuala ya uwezeshaji kiuchumi; na
- Kusimamia na kufuatilia utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Sehemu ya Maudhui ya Ndani “Local Content”
Sehemu hii itatekeleza majukumu yafuatayo: -
- Kuandaa na kupitia Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo, Mikakati, Programu, na Miradi kuhusu masuala ya ushiriki wa watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji inayotekelezwa nchini;
- Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo kuhusu masuala ya ushiriki wa watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji inayotekelezwa nchini;
- Kuratibu ujumuishaji wa masuala ya ushiriki wa watanzania katika Sera, Sheria, Kanuni, Mikakati na Miradi ya Wizar ana Taasisi za Kisekta;
- Kufuatilia na kutathmini viwango na utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo inayohusu ushiriki wa watanzania katika Wizara za kisekta, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
- Kukuza ushiriki wa watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji inayotekelezwa nchini;
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kuhusu masuala ya ushiriki wa watanzania;
- Kukuza ushiriki wa watanzania katika Wizara zote za kisekta, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuweka mazingira wezeshi yatakayowawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika mnyororo wa thamani wa shughuli za kiuchumi;
- Kusimamia masuala yote yanayohusu ushiriki wa watanzania yanayotekelezwa na sekta binafsi kwa kushirikiana na Wizara za kisekta;
- Kuratibu utoaji na uimarishaji wa mazingira wezeshi ya ushiriki wa wazawa katika Wizara zote za kisekta;
- Kuratibu tafiti na tathmini kuhusu masuala ya ushiriki wa watanzania pamoja na kupendekeza hatua za kuimarisha ukuaji wake;
- Kuzisaidia Wizara za kisekta kuweka viwango vya matumizi ya malighafi, bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini, pamoja na masharti ya kuzuia matumizi ya vile vinavyoweza kupatikana ndani ya nchi;
- Kusimamia na kutoa miongozo ya utekelezaji wa masuala ya ushiriki wa watanzania kwa Sekta Binafsi;
- Kusimamia ushiriki wa watanzania katika manunuzi ya umma yanayofanywa na taasisi nunuzi zikiwemo Wizara na Taasisi za kisekta, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
- Kuhamasisha na kuimarisha Majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika ngazi zote kupitia Mabaraza ya Biashara ya Wilaya (DBCs), Mabaraza ya Biashara ya Mikoa (RBCs), Mabaraza ya Majadiliano kati ya Wizara na Sekta Binafsi (MPPD) na Baraza la Taifa la Biashara (TNBC);
- Kuratibu, kusimamia na kutathmini utekelezaji wa maazimio ya mikutano ya mabaraza ya Wilaya (DBCs), Mikoa (RBCs), Wizara (MPPD) na TNBC; na
- Kusimamia na kufuatilia utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC).




