Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Wito watolewa wananchi kutembelea banda la OWM maonesho ya wiki ya utumishi


Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu kupitia Wakala wa Serikali wa Uchapaji Tanzania inawaalika wananchi kutembelea Banda la Ofisi hiyo kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi ili kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa ikiwemo uchapishaji wa  Sheria, Kanuni, Katiba ya Tanzania, machapisho mbalimbali ya vitambulisho vitambulisho, vyeti na nyaraka zote za kiserikali.

Wito huo umetolewa leo katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma na Afisa Biashara Bi. Witness  Njunde kutoka Wakala wa Serikali wa Uchapaji Tanzania wakati akizungumzia kuhusu huduma zinazotolewa na Wakala huyo wa Serikali.

Bi. Njunde amesema “Moja ya kazi tunazofanya ni kuchapisha  gazeti la Serikali, Gazeti hili la Serikali limebeba maudhui ambayo ni ya kiserikali na kibinafsi. Katika maudhui ya kibinafsi huwa linatangaza mabadiliko ya majina, mirathi, kupotea kwa leseni za makazi, kufungwa kwa makampuni hali kadhalika pindi mtu anapopotelewa na vyeti vyake vya shule, passport, leseni zote hizo tunatangaza katika gazeti la serikali”.