Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Serikali yaendeleza jitihada kuhakikisha Wenye Ulemavu hawaachwi nyuma katika maendeleo ya Taifa.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga amebainisha jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ikiwemo  ukamilishwaji wa Mfumo tambuzi wa Kielektroniki wa taarifa za Watu wenye Ulemavu (PD-MIS).

Pamoja na mahitaji ya msingi ya Wenye Ulemavu yanayoendelea kutolewa, Serikali pia imeweka vipaumbele kwa Wenye Ulemavu katika ajira, elimu, afya sambamba na Mpango wa kunusuru Kaya Masikini (TASAF) ambao unajumuisha Kaya za Wenye Ulemavu kama kigezo kimojawapo.

Naibu Waziri amebainisha hayo kwenye kikao na wajumbe wa Shirika lisilo la Kiserikali  Patronage Center for Persons with Disability (PPD), kilichofanyika leo katika ukumbi mdogo wa Waziri Mkuu Ngome Jijini Dodoma.