Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Kabudi, ahimiza matumizi ya teknolojia za kisasa katika uzalishaji


Washiriki wa Maonesho ya nane watakiwa kuendelea kuzingatia ubunifu, teknolojia mpya katika shughuli zao za uzalishaji ili zisaidie katika kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa kazi.

Kauli hiyo Imetolewa leo  Mkoani Morogoro na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Mhe, Prof. Palamagamba Kabudi wakati akifunga maonesho ya nanenane Kanda ya Mashariki.

Waziri amehimiza viongozi wa Mikoa kuhakikisha teknolojia zilizooneshwa kwenye viwanja vya Nanenane zinafikishwa kwa wananchi kupitia huduma za ugani na mashamba darasa.

“tuendelee kutumia Jukwaa la Business-to-Business (B2B) ili liweze kkuweka malengo yanayopimika katika biashara, uwekezaji na masoko” alihimiza Waziri Kabudi

Aidha  taasisi  nyingine kama ( TBS), (SIDO) ziendelee kujikita katika kuwasaidia wajasiriamali wadogo kufikia viwango vinavyohitajika kushindana katika soko la ndani na nje ya nchi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa utumishi wake wa kipekee katika taifa na kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa alieleza, “Maonesho ya Mwaka yamefanyika yakiwa katika utekelezaji wa mwaka wa kwanza wa dira ya taifa 2050, nasi tumeondoka katika mafanikio ya maonesho kwa kuangalia idadi ya mabanda na sasa tumeweka vigezo maalumu kwa kuangalia elimu iliyotolewa na teknolojia iliyochukuliwa na muunganiko wa biashara iliyopatikana.”

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Batlida Burian amempongeza Mhe, Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kusainiwa kwa mkataba wa kiwanda cha Usafishaji Mafuta Mkoani Tanga.

“Mhe, Rais ameshaacha tabasamu kabla ya kufika mwaka 2030 mradi huo mkubwa utawezesha kunufaisha Tanga na kanda nzima ya Mashariki, tumejipanga kuhakikisha kila mtu ananufaika na fursa hii ya ujengwaji wa kiwanda ambayo imetolewa,”alibainisha