Habari
Ofisi ya Waziri Mkuu yashiriki maadhimisho ya mei mosi 2026 Dodoma
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) wameungana na watumishi wengine wa Serikali kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani leo, Mei 1, 2026, katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, ambapo alisisitiza umuhimu wa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kujituma ili kuchochea maendeleo ya taifa.
Amesema kuwa mchango wa wafanyakazi ni msingi muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya nchi, hasa katika kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Kazi Zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050”, ikilenga kuhamasisha mazingira bora ya kazi na ustawi wa wafanyakazi nchini.




