Habari
Dkt. Biteko ashiriki hafla ya kupokea gawio na michango kutoka kwa Taasisi na Mashirika ya Umma
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameshiriki katika hafla ya kupokea gawio na michango kutoka kwa Taasisi na Mashirika ya Umma na Kampuni ambazo Serikali ina hisa zake.
Hafla hiyo imefanyika Juni 10, 2025 Ikulu jijini Dar es salaam na kupokelewa na mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.