Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

NBC yatoa mkono wa pole kwa waathirika wa maafa Hanang


Uongozi wa Banki ya NBC Umetoa salamu za pole kwa waathirika wa Maafa ya Maporomoko ya tope na mawe Hanang kwa kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni Kumi Pamoja na misaada ya kibinadamu ikiwemo; vyakula (unga wa sembe,maharage, mchele na mafuta ya kupikia.

Pamoja na hivyo watumishi wa banki hiyo wametoa nguo, mablanketi na mashuka ili kuendelea kusaidia waathirika hao walioko katika Kambi tatu katika Halmashauri ya Hanang mkoani Manyara.

Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NBC, Godwin Jaha amesema banki imechangia mara baada ya kuguswa na tukio la maafa hayo huku akiahidi kuwa banki itaendelea kuungana na Serikali ili kuhakikisha waliofikwa na maafa hayo wanarejea katika hali zao kama ilivyokuwa awali.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewashukuru na kuupongeza uongozi wa banki hiyo.

=MWISHO=