Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Majukumu

Ofisi ya Waziri Mkuu inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Hati ya Mgawanyo wa Majukumu ya Mawaziri (Presidential Instrument). Kwa mujibu wa Hati hiyo, majukumu mahsusi ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni haya yafuatayo: -

 1. Kuratibu Sera na Shughuli za Serikali;
 2. Kuongoza na kuratibu Shughuli za Serikali Bungeni;
 3. Kiungo kati ya Vyama vya Siasa na Serikali ;
 4. Kuratibu Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa ;
 5. Kusimamia na Kuratibu Shughuli za Dharura na Maafa;
 6. Kuchapisha Nyaraka za Serikali;
 7. Kuratibu na Kusimamia Maendeleo ya Sekta Binafsi na Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi;
 8. Kuwezesha utekelezaji wa Mpango wa uendelezaji wa Mji wa Dodoma kama Makao Makuu ya Tanzania na kuratibu uhamiaji wa Serikali Dodoma;
 9. Kuratibu na Kusimamia Shughuli za Baraza la Taifa la Biashara;
 10. Kuratibu Shughuli za Kudhibiti Maambukizi ya UKIMWI; 
 11. Kuratibu shughuli za kudhibiti uingizaji na matumizi ya Dawa za Kulevya; na
 12. Kuratibu na kuwezesha Shughuli za Uchaguzi.