Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Jingu aongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu ameongoza kikao cha 8 cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi kilicholenga kupokea taarifa ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 iliyofanyika  tarehe 23 Agosti, 2022 pamoja na kujadili Rasimu ya Mwongozo wa Matumizi ya Takwimu ya Sensa ya Watu na Makazi nchini.

Kikao hicho kilifanyika tarehe 27 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Julius Nyerere Interational Covention Centre Jijini Dar es Salaam (JNICC).

Jukumu kubwa la Kamati hiyo ni kuishauri Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa inayoongozwa na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar namna bora ya utekelezaji wa masuala ya sensa.