Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Jingu aongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 Dar es Salaam.


Kamati ya Ushauri ya Sensa ya Watu na Makazi imefanya kikao kazi cha utekelezaji wa Sensa ya Mwaka 2022. Katika kikao hiki, Kamati imepokea taarifa ya hali ya maandalizi kuelekea Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 itakayofanyika tarehe 23 Agosti, 2022.

Jukumu kubwa la Kamati ya Ushauri ni kuishauri Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa inayoongozwa na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar namna bora ya utekelezaji wa Sensa.

Aidha kikao kilifanyika tarehe 04 Juni, 2022 katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam.

Kaulimbiu ya Sesa ya Watu na Makazi 2022 ni “Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa”