Habari
Waziri Simbachawene aongoza kikao cha Mawaziri
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameongoza kikao cha Mawaziri kwa lengo la kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za makazi.
Kikao hicho kimefanyika Mei 27, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma ambapo kilihudhuriwa na mawaziri wakiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Nchi Ofisi wa Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angelina Mabula.
Kikao hicho kimefanyika kama sehemu ya maandalizi ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 2022 nchini ambapo itakuwa Sensa ya Sita tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 na sensa ya watu na makzi hufanyika kila baada ya miaka 10.
####MWISHO####