Habari
Wananchi waombwa kuendelea kulinda amani na mshikamano wa kitaifa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuzilinda tunu za umoja wa kitaifa za utulivu, amani na ushirikiano.
Rai hiyo ametoa wakati akimwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Katika Misa ya kuweka wakfu Askofu wa Jimbo la Njombe Dkt. Eusebius Samwel Kyando iliyofanyika Mkoani Njombe
Waziri amesema kuwa tunu hizo ndizo zinazotambulisha Taifa letu la Tanzania duniani na ulimwenguni kote.
"Tunu hizi zilindwe kwa kuzingatia umuhimu wake, pia Serikali inashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuliombea Taifa, tunaomba muendelee kuliombea bila kuchoka " alifafanua Waziri
Aidha viongozi wa dini mmekua mstari wa mbele kuhakikisha Taifa hili linaendelea kuwa katika hali ya utulivu mstahimilivu na Mhe. Rais amekuwa mstari wa mbele Kati Jambo hilo.
"Niwaombe Sana Viongozi wa dini tuendelee kukemea pale tunapoona kuna viashiria vya watu wachache kuvunja amani, utulivu umoja na mshikamano wa Nchi yetu," alihimiza
Aidha aliitaka jamii kuungana na Serikali katika kupaza sauti juu ya matendo maovu na hasa mauaji na ukatili wa kijinsia, imani potovu ambazo zinapelekea mauaji na unyanyasaji wa watoto.
Aliongezea kuwa Falsafa ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani ya 4R, inalenga sekta zote na utendaji wote ndani ya serikali, na utendaji wa waumini na taasisi zake za kidini hivyo, aliwaombe viongozi wa dini kuunga mkono falsafa hiyo hasa katika ustahimilivu na maridhiano.
"Dhamira ya Mhe. Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani ni njema na inahitaji kutiwa moyo ili iweze kusonga mbele hasa kwa vitendo," alisisitiza
Akizungumza kuhusu masuala ya uchaguzi na fursa zilizopo aliisihi jamii kuwa tayari kuitumia kwa kushiriki vyema uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024.
“Uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka huu 2024, niwaombe wananchi tuweze kushiriki zoezi la uchaguzi huo kwa amani na utulivu,” aliongeza
Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony Mtaka ameomba viongozi wa dini kwa kushirikiana na serikali kwa pamoja kuunga mkono jitihada zinazofanywa katika sekta ya elimu hasa katika masuala ya lishe kwa wanafunzi mashuleni katika kukabiliana na tatizo la utapiamlo.
"Hii itasaidia kuleta hamasa kuwaandaa watoto kwa kuwapatia lishe Bora ambayo itawasaidia kufanya vizuri katika maisha yao,"Alisema.
Kwa upande wake mmoja wa waumini wa kanisa hilo Bi, Naomi Nzota amesema waumini wa Jimbo la Njombe wamefurahi Sana kwa kupata Askofu Dkt. Eusebius Kyando baada ya Misa wa kuweka wakfu iliyoongozwa na Muasham Askofu Mstaafu wa Jimbo la Dar es salaam Polcapy Pengo.
"Ameueleza utumishi wa Askofu Dkt. Eusebius Kyando kwamba ni mtumishi, mnyenyekevu mnyoofu na mvumilivu," alieleza