Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Tanzania yashiriki Jukwaa la Nane la Dunia la upunguza Madhara ya Maafa Geneva


TANZANIA imeshiriki Jukwaa la Nane la Dunia la Kupunguza Madhara ya Maafa ili kutathmini, kujadili maendeleo ya utekelezaji wake na kuimarisha masuala ya usimamizi wa maafa kimataifa kupitia makubaliano ya hiyari ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo yameridhiwa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameongoza ujumbe kutoka Tanzania kushiriki katika mkutano huo Mjini Geneva, Uswisi kuanzia tarehe 02 hadi 6 Juni 2025.