Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Serikali yahimiza ushirikiano katika kuimarisha utendaji wa kazi sekretarieti ya SADC


Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameishauri sekretarieti ya SADC kwa Kushiriiana katika kuimarisha  utendaji wa kazi wa Kituo cha udhibiti wa Maafa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu katika Mkutano wa kamati ya Mawaziri wanaoshughulika na udhibiti wa maafa kwa Nchi wanachama wa SADC uliofanyika Lilongwe Nchini Malawi.

Katika kikao hicho waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu aliaambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya waziri Mkuu Meja Jenerali Michaeli .M. Mumanga aliyeongeoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao hicho.