Habari
Serikali kuwekeza katika uvuvi wa bahari kuu
Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Paul Sangawe ameongoza Kikao cha Kamati ya Wataalamu kuhusu matokeo ya tathmini ya kazi ya tafiti juu ya kampuni zenye uwezo wa kujenga Meli kwa ajili ya Uvuvi katika Bahari Kuu.
Katika Kikao hicho, Bw. Sangawe alilisitiza juu ya utekelezaji wa maelekezo ya Kikao cha Kamati ya Usimamizi wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi kilichofanyika kabla ya kikao cha wataalam. Masuala yaliyosisitizwa ni pamoja na upatikanaji kampuni yenye uwezo wa kujenga Meli ya Uvuvi wa Bahari Kuu kwa viwango vinavyohitajika, na kupata meli hizo kwa wakati ili kuchochea uvuvi wa kisasa nchini.
Vikao hivyo vya Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi ( AFDP) vimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Bluu, Zanziba