Habari
Rais wa Jamhuri ya watu wa Sahrawi atembelea Mji wa serikali Mtumba
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Sahrawi, Mhe. Brahim Ghali leo amefanya ziara ndogo katika mji wa Serikali Mtumba ambapo alitembelea jengo la Ofisi ya Rais Menejiment na Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Katika ziara hiyo ndogo Mhe. Rais Brahim Ghali alikaribishwa na kuoneshwa Mji wa Serikali na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Uratibu Bwn. Omar S Ilyas, pamoja na Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Bwn. Meshack Bandawe, ambapo walipata nafasi ya kuonyeshwa kiwanja cha Ubalozi wa Taifa la watu wa Sahrawi.