Habari
Parokia ya Kiwanja cha Ndege yawakumbuka waathirika Hanang
Padre Emmanuel Mtambo wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowaska amesema Kanisa linawajibu wa kuchangia watanzania wenzetu waliopata janga la mafuriko ya Mawe na Matope kutoka Mlima Hanang’.
Alisema Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowaska Kiwanja cha Ndege kupitia kamati ya Caritas ambayo inashughulikia wanaohitaji, leo jijini Dodoma imetoa hundi ya shilingi milioni 5 ikiwa ni sehemu ya kushirikiana na serikali kusaidia waathirika.
“Kama Parokia na Kanisa; tunapaswa kufanya sehemu yetu, kupitia michango yetu tunayotoa katika akaunti ya Caritas” alifafanua
Mchango huo umepokelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama.