Habari
Naibu Waziri Ummy ashiriki ibada ya kuaga mwili wa Marehemu William Lukuvi
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akiwa katika ibada ya kuaga mwili aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi leo tarehe 28 Machi, 2026 katika viwanja vya Karimjee Hall Jijini Dar es salaam.
Mhe. Lukuvi amefariki dunia tarehe 25 Machi, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Mkoani Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.




