Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Naibu Waziri Nderiananga ametembelea na kufanya mazungumzo na viongozi wa mkoa wa Arusha


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiw Ummy Nderiananga amewasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kupokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Missaille Albino Musa leo Novemba 4, 2024.

Mhe. Nderiananga licha ya kusaini kitabu cha wageni amefanya mazungumzo na Katibu Tawala huyo kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa pamoja na uwajibikaji na utekelezaji wa shughuli za Serikali mkoani humo.

Aidha, Mhe. Nderiananga yuko mkoani Arusha kwa lengo la kuhudhuria Mkutano wa Afya Moja Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) ukumbi wa Nyasa.

Mkutano huo unafanyika kuanzia tarehe 04 hadi 06 Novemba, 2024.

 

=MWISHO=