Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Maonesho ya vyuo ni tija kwa wananchi katika kukuza elimu ujuzi


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya amevipongeza Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kutoa maarifa  mbadala kwa changamoto zinazoikabili jamii. Hii inatoa hamasa kwa sababu wanaungana na sera za nchi katika kuongeza fursa za kupata ajira.


“Mafunzo ya Elimu ya ufundi na Mafunzo ya ufundi Stadi yanagusa eneo muhimu sana la vijana, vijana wengi wamepata elimu hii kwa mafunzo ya muda mfupi miezi mitatu, miezi sita, miaka mitatu ambayo yanawawezesha kupata ujuzi mbalimbali katika utendaji kazi  pamoja na kutoa vyeti.”


 Amesema hayo alipotembelea Maonesho ya Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi yanayofanyika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma ambayo yamesaidia  kutoa maarifa kwa wananchi kujua fursa za ajira zilizopo katika maeneo yao, lakini pia kusaidia wataalamu wetu kuwa na maarifa yanayoendana na soko la ajira linalohitajika katika Nchi yetu
Naibu katibu mkuu Mmuya ametoa rai kwa wanavyuo na  wakufunzi kuendelea kuangalia mahitaji ya jamii ili waweze kuandaa mafunzo ya muda mfupi  ili kuweza kuwapatia wananchi ujuzi unaotakiwa utakaosaidia kuzalisha ajira nyingi.


Naye Mkurugenzi mtendaji wa mitala na upimaji Dr. Annastelllah Sigweyo amesema baraza inaangalia program zinazoanzisha zainaendana na uhitaji wa jamii baada ya kufanya utafiti wa eneo husika na kwa kuzingatia ushauri wa wadau.
tunaangalia uwezo wa chuo kinachotaka kutoa program kama kina uwezo wa kutoa ujuzi husika kwa kuangalia uwezo wa walimu kitaaluma katika kutoa ujuzi, ndipo tunapopitisha mtaala kwa ajili ya chuo husika.