Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Yonazi aongoza kikao cha Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM)


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) ambaye pia ni Mwenyekiti wa TNCM inayosimamia utekelezaji wa Programu zinazofadhiliwa na Mfuko wa Dunia (Global Fund) Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha wajumbe wa chombo hicho kwaajili ya kujadili utekelezaji wa program za Malaria, Kifua Kikuu, UKIMWI pamoja na uimarishaji wa mifumo ya kutolea huduma za Afya nchini kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia kwa kipindi cha mzunguko wa 7 (GC7) kuanzia mwaka 2024 - 2026.

Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.