Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Yonazi aongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha 12 cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kilichohusu Kujadili Taarifa ya Maendeleo ya Utekelezaji wa Awamu ya Tatu na ya Mwisho ya Sensa ya Watu na Makazi  ya Mwaka 2022. Taarifa hii ni ya kipindi cha Desemba, 2023 hadi Mei, 2024. Kikao hicho kilifanyika katika  Ukumbi wa Julius Nyerere Interational Covention Centre (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Juni, 2024