Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt.Yonazi akutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa TPSF


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na  uongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Raphael Maganga lengo ni kujitambulisha kwa katibu Mkuu huyo pamoja na kuzungumzia vipaumbele vya Taasisi hiyo, masuala ya kuendeleza sekta binafsi, kutambua fursa za biashara nje ya nchi pamoja na kubainisha vipaumbele vya taasisi na maeneo ya kuimarisha ushirikino na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Uongozi huo umemtembelea tarehe 14 Juni, 2024 Jijini Dodoma.