Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Yonazi aipongeza Muhimbili kupeleka msaada wa msaikolojia tiba, dawa na vifaa tiba Hanang’


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameipongeza uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kupeleka msaada wa dawa, vifaa tiba pamoja Msaikolojia Tiba kwa wananchi wa  Mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang, Mkoani Manyara ili kusaidia jitihada za utoaji huduma.

Eneo hilo, lilikumbwa na maafa ya maporomoko ya tope na mawe kutoka mlima Hanang’ na kuleta madhara makubwa ikiwemo vifo, majeruhi, upotevu wa mali na uharibifu wa miundombinu.

Dkt. Yonazi amesema MNH imepeleka mchango ambao una aina mbalimbali (varieties) na kuwataka wengine kuiga mfano huo.

“Muhimbili mmefanya vizuri kwa kuungana nasi kuhakikisha wagonjwa wanapatiwa matibabu na vifaa tiba muhimu hii imeonesha namna mnaavyojali na hakika Taifa letu limeendelea kuwa na umoja na mshikamano katika nyakati tofauti tofauti ikiwemo huu wa  maafa,” alisema Dkt. Yonazi

Akikabidhi dawa na vifaa tiba, Msaikolojia Tiba kutoka MNH Bi. Egla Fugusa amesema msaada huo una thamani ya TZS. 38 Mil.

“Kwa niaba ya Mkurugenzi wetu ametupa majukumu ya kuja kutoa huduma za kisaikolojia huku na hii tutaifanya kwa uadilifu mkubwa kwa ajili ya kusaiodia wenzetu huku Hanang’,” alisisitiza Egla

=MWISHO=