Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Biteko awasili Rwanda kushiriki Mkutano wa Nyuklia Afrika


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt Doto Biteko Juni 29, 2025 amewasili Kigali nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano unaohusu masuala ya nyuklia Afrika.

Katika Mkutano huo unaotarajiwa kuanza Juni 30 hadi Julai 1, 2025  nchini humo unajumuisha wadau wa nishati kutoka ndani na nje ya Afrika wenye lengo la  kuharakisha  matumizi ya nyuklia kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuleta mabadiliko ya nishati Afrika.

Pamoja na ushiriki wake katika Mkutano huo Dkt. Biteko anatarajiwa kufungua mjadala wenye mada kuhusu nishati Afrika na utashi wa kisiasa.

Aidha, katika Mkutano huo Dkt. Biteko ameambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na Mkurugenzi wa Tume ya Mionzi ya Atomiki, Prof. Najat Mohamed.

Awali alipowasili nchini Rwanda, Dkt. Biteko alipokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uchukuzi wa  nchini humo, Mhe. Olivier Kabera.

Mwisho