Habari
Dkt. Biteko atoa maoni Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na Timu ya Uandishi wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 kwa ajili ya kutoa maoni yake.
Dkt. Biteko ametoa maoni hayo Oktoba 28, 2024 ofisini kwake jijini Dodoma ambapo amebainisha maeneo kadhaa yanayohitaji kuzingatiwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ili kusaidia kuchochea maendeleo na ustawi wa Taifa.
Baadhi ya maeneo hayo ni kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuweka misingi imara katika sekta mbalimbali ili kuendana na mahitaji na ukuaji katika sekta husika