Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Biteko ashiriki uzinduzi wa Taarifa ya Maboresho ya Mazingira ya Uwekezaji na Biashara


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameshiriki katika Uzinduzi wa Taarifa za Maboresho ya Mazingira ya Uwekezaji na Biashara na Nyenzo za Usimamizi wa Uwekezaji Nchini uliofanyika leo Septemba 11, 2024 katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo umeongozwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mjumbo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila pamoja na Viongozi mbalimbali.