Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Waziri Simbachawene atembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu


Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (Mb) leo June 17, 2025 ametembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu lililopo katika maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) ikijumuisha idara na taasisi zilizo chini yake inashiriki maonesho hayo.