Wenye Ulemavu
KITENGO CHA WATU WENYE ULEMAVU
LENGO KUUU:
Kukuza haki na ustawi wa Watu wenye Ulemavu katika nyanja zote za maisha.
MAJUKUMU YA KITENGO CHA WATU WENYE ULEMAVU
- Kuandaa na kufanya mapitio ya sera, sheria na miongozo kuhusu masuala ya Watu wenye Ulemavu;
- kuratibu uanzishaji na uendelezaji wa programu za marekebisho na huduma za utengamao kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu;
- Kuendeleza na kuratibu mipango endelevu ya uwezeshaji kwa Watu wenye Ulemavu;
- Kuratibu, kufuatilia, kutathmini na kufanya mapitio ya makazi, huduma na matunzo kwa Watu wenye Ulemavu;
- Kuratibu na kutoa huduma za ushauri kwa vyama vya Watu wenye Ulemavu na vinavyowahudumia Watu wenye Ulemavu, pamoja na mashirika ya Kitaifa na Kimataifa yanayotoa na/au kujihusisha na huduma kwa Watu wenye Ulemavu;
- Kuratibu na kufanya ufuatiliaji wa utoaji wa huduma za ustawi wa jamii kwa Watu wenye Ulemavu;
- Kuratibu na kufanya tafiti na tathmini ya athari za afua mbalimbali kwa Watu wenye Ulemavu;
- Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa mikataba, itifaki na makubaliano ya kimataifa na kikanda kuhusu haki na ustawi wa Watu wenye Ulemavu.




