Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Waziri Lukuvi ashiriki mapokezi ya mwili wa Dkt. Faustine Ndugulile


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa William Lukuvi ameungana na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na waombolezaji, wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki wakati wa kupokea mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni ambaye pia ni Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile ulipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tarehe 29 Novemba, 2024.

Viongozi mbalimbali wameshiriki katika mapokezi ya mwili huo wakiwemo Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge, Waheshimiwa Wabunge, Katibu wa Bunge na Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi.

Mwili wa Marehemu Mhe. Dkt. Ndugulile umehifadhiwa katika Hospitali ya JWTZ Lugalo na unatarajiwa kuzikwa tarehe 3 Disemba, 2024 katika eneo la familia Mwongozo, Wilayani Kigamboni.

 

=MWISHO=