Habari
Uzinduzi wa mfumo wa anuani za makazi Zanzibar wafana
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga, ameshiriki katika hafla ya uzinduzi wa mfumo wa anuani za makazi, unaolenga kutoa huduma ya barua ya utambulisho wa mkazi kwa njia ya kidijitali.
Uzinduzi huo umefanyika leo katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, ukiongozwa na Mgeni Rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Ummy amepongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa jitihada zao za kuimarisha huduma za kijamii kupitia mifumo ya kidijitali.
"Niwapongeze kwa kuendelea kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa urahisi zaidi kupitia teknolojia. Mfumo huu utarahisisha utambuzi wa makazi na uboreshaji wa utoaji wa huduma mbalimbali serikalini," alisema Mhe. Ummy.
Aidha, amezipongeza wizara zote za kisekta kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano wao uliowezesha utekelezaji wa mfumo huo muhimu kwa maendeleo ya Taifa