Habari
Serikali yapongezwa kuendelea kuongeza afua za UKIMWI
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Elibariki Emmmanuel Kingu ameipongeza Serikali na wadau wa maendeleo wanaoshirikiana na Serikali katika kutoa afua mbalimbali kukabiliana na ugonjwa wa Virusi vya UKIMWI.
Ameeleza umuhimu wa Semina hiyo katika kutambua wadau wanaoshirikiana na Serikali kwa karibu na kuishauri serikali katika kuongeza muitikio wa kisiasa wa kuendelea kushawishi wadau hao kuwa na mkakati stahimilivu katika kusaidia afua za UKIMWI.