Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Rais Dkt. Samia na Rais Nyusi ndani ya banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sabasaba


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakati akitoa maelezo kuhusu Mfumo wa Ufuatiliaji wa mwenendo wa majanga na tahadhari ya mapema (MYDEWETRA) wakati

walipotembelea katika Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizochini yake  katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) tarehe 03 Julai, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Maonesho hayo ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam (Sabasaba) yamefunguliwa rasmi leo (Julai 3, 2024) na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi pamoja na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.