Habari
Miaka 50 ya maonesho ya sabasaba wananchi wakaribishwa kupata elimu banda la Waziri Mkuu
Mkurugenzi wa Idara ya Uwezashaji Kiuchumi na Maudhui ya Ndani Bw. Condrad Millinga ametoa wito kwa wananchi kutembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba kwaajili ya kupata elimu.
Bw. Millinga ameongeza kuwa banda hilo linajumuisha Taasisi na Idara zote ambazo zipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu hali itakayowasaidia wananchi kupunguza kutembea sana kutafuta Ofisi mojamoja, wito huo ameutoa ikiwa ni siku ya Ufunguzi Rasmi wa maonyesho hayo.
Ambapo mgeni rasmi katika siku hii ya ufunguzi atakuwa Rais wa Msumbiji Mhe. Daniel Francisco Chapo, akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan




