Habari
Majaliwa kumwakilisha Rais Dkt. Samia uapisho wa Rais Rajoelina
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Disemba 15, 2023 amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ivato uliopo Antananarivo nchini Madagascar na kupokelewa na Waziri Mkuu wa Madagacar, Christian Ntsay.
Mheshimiwa Majaliwa kesho Disemba 16, 2023 atamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sherehe za kumwapisha Rais wa nchi hiyo, Andry Rajoelina zitakazofanyika kwenye uwanja wa Mahamasina Barea Stadium uliopo Antananarivo.
Mheshimiwa Rajoelina ameshinda nafasi hiyo kwa muhula wa tatu kwa asilimia 58.9 ya kura zilizopigwa akifuatiwa na Siteny Randrianasoloniaiko ambaye alipata asilimia 14.39 ya kura zilizopigwa
Mheshimiwa Majaliwa amefuatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masala ya Afrika ya Mashariki Wakili Stephene Byabato na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Eswatin na Madagascar, Phaustine Kasike.