Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Yonazi ateta na Menejimenti ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Nchini


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) mapema Machi 10, 2023 katika ukumbi wa mikutano Ofisi hiyo Jijini Dodoma.

Lengo la kikao hicho ni kumpitisha Katibu Mkuu huyo kuhusu Muundo na utendaji wa Tume ikiwa ni sehemu ya ratiba yake kukutana na Idara na Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Dkt. Yonazi alitumia nafasi hiyo kuipongeza Tume kwa kazi nzuri wanazofanya na kuwaeleza ni muhimu kuongeza kasi zaidi katika kuyafikia malengo na kuhakikisha jamii inapata huduma na elimu kadiri iwezekanavyo.

 “Ninawapongeza TACAIDS kuendelea kusaidia katika mapambano haya na kila jitihada zinazofaywa zina tija katika kuyafikia malengo hivyo, tuendelee kutoa elimu kwa umma kwa kuzingatia kuwa mnayagusa maisha watu,”alisema Dkt. Yonazi

Aliongezea kuwa, Ofisi yake ipo wazi na itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tume hiyo kwa kuzingatia umuhimu wa shughuli zinazotekeleza na Tume.