Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Yonazi aongoza kikao cha kujadili changamoto za kiwanda cha TBPL


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameongoza Kikao cha Makatibu Wakuu cha kujadili changamoto zinazokabili Kiwanda cha Kuzalisha Bidhaa za Kibaiolojia cha Tanzania Biotech Products Limited (TBPL - Viuadudu) kilichofanyika tarehe 31 Oktoba, 2024 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.