Habari
Dkt. Biteko na Waziri Aweso wakutana kujadili utendaji kazi wa sekta zao
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Wizara ya Maji kwa lengo la kujadili namna ya kuboresha utendaji kazi na kukabiliana na changamoto zinazozikabili Taasisi zilizoko chini ya Wizara hizo. Kikao hicho kimefanyika leo Januari, 23, 2025 jijini Dodoma.