Habari
Dkt. Biteko ashiriki Hafla ya Kumtunuku Tuzo ya Heshima Rais Dkt. Samia
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameshiriki katika hafla maalum ya utoaji wa Tuzo ya heshima ya Taifa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, iliyofanyika katika Viwanja vya Bunge, jijini Dodoma, Mei 31, 2025.
Tuzo hiyo ya heshima imetolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Tulia Ackson, kwa niaba ya wananchi wote wa Tanzania, ikiwa ni kutambua na kuthamini mchango mkubwa wa Mhe. Rais Samia katika kuleta maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidiplomasia nchini, pamoja na uongozi wake mahiri wa kuleta mshikamano kitaifa.
MWISHO