Habari
Dkt. Biteko afanya mazungumzo na balozi wa India nchini
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Septemba 21, 2024 ofisini kwake jijini Dar es salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey.
Katika mazungumzo yao Dkt. Biteko amesema kuwa Tanzania ipo tayari kuendelea ushirikiana na India katika masuala ya nishati.
Kwa upande wake, Balozi Dey amesema kuwa Tanzania ni mdau muhimu katika masuala ya nishati barani Afrika na hivyo nchi yake itaendelea kuangalia maeneo ya kushirikiana katika miradi ya nishati.
Aidha, Balozi Dey amemualika Dkt. Biteko kushiriki katika Wiki ya Nishati ya India inayotarajiwa kufanyika mapema mwakani.
=MWISHO=