Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Biteko achangia Azimio la Bunge la kumpongeza Rais Samia


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko Januari 31, 2025 amechangia Azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nishati Afrika (Mission 300) uliyofanyika Januari 27 na 28, 2025 jijini Dar es Salaam.

“Wabunge mmeonesha uungwana mkubwa sana kwa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusukuma mipango ya Serikali kwa ajili ya kuwahudumia wananchi lakini pia Bunge hili limethibitisha uungwana na ustarabu na leo tunakuunga mkono, tunakutia moyo, tunakuombea, tunakutakia mema. Matashi  yetu kwa Rais wetu ni kuona Tanzania inaendelea, ”  amesema Dkt. Diteko.

MWISHO