Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Waziri Simbachawene, ampongeza Mama Tunu Pinda


Kuimba kuna nguvu kubwa; kuimba ni kusali mara mbili, wenzetu mmekuewa watumishi wa Mungu kwa njia ya uimbaji na kazi mnayoifanya ya utume inawasaidia mpate neema na baraka kubwa.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Mtakatifu Theresia, wa Mtoto  Yesu inayoitwa Mungu asiye shindwa iliyofanyika katika Parokia ya Nzinje Mjini Dodoma.

“Kwaya hii ya Mtakatifu Theresia, Mtoto yesu ndio anayoimbia Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda, amechagua jambo zuri sana la kufanya baada ya Kustaafu”.