Habari
Waziri Mkuu atimiza ahadi ya kumpatia Kitimwendo Helena Joseph
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo (Aprili 20, 2026) amemkabidhi kitimwendo Helena Joseph Mwandu (mwenye mahitaji maalum), Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri Mkuu aliahidi kumpatia Helena kiti hicho katika mazungumzo waliyoyafanya baada ya mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Msanga wilayani Chamwino Dodoma, jana (Aprili 19, 2026).
Akizungumza baada ya kupatiwa kiti hicho, Helena amemshukuru Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu kwa kumpatia kitimwendo hicho kwani kitamsaidia katika shughuli zake.




