Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Waziri Mhagama Ashiriki mkutano wa kujadili hali na athari za mvua za El nino katika ukanda wa SADC.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ameshiriki katika Mkutano wa kujadili hali na athari za mvua za El Nino katika Ukanda wa SADC.

Mkutano huo ulifanyika  kwa njia ya Mtandao (Zoom meeting)   Jijini Dodoma ukihusisha Wizara za Kisekta  zinazohusika na Masuala ya Kilimo, Maji, Nishati na Uratibu wa udhibiti wa Maafa ni maandalizi ya Mkutano wa dharura wa Wakuu  wa Nchi na Serikali  wa Jumuiya ya Maendeleo ya  Kusini mwa Afrika (SADC) Kuhusu Hali ya Mvua za El nino utakaofanyika kwa njia ya Mtandao Mei 20, 2024.