Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Wananchi wapewa rai kujitokeza kupima kwa hiari VVU


Wito umetolewa kwa wananchi kuendelea kujitokeza kupima VVU kwa hiari ili kujua hali zao ili kuendelea kuishi kwa kuzingatia matokeo, kwa wale ambao hawatakutwa na maambukizi ni nafasi kwao kuendelea kuishi ili wasiambukizwe na wale ambao watakutwa na maambukizi  wana nafasi kuendelea kuishi kwa kutumia dawa za kufubaza.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa kikao cha pamoja Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Adam Kighoma Malima kuhusu kuelekea maandalizi ya siku ya UKIMWI kitaifa, katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Ameongeza kusema tafiti zote za miaka mitano zimeonesha wanaume hawajitokezi kupima, na hawajitokezi kuanza kupata dawa, na hivyo kusumbuliwa sana na magonjwa Nyemelezi yanayotokana na virusi vya UKIMWI.

“Virusi vya UKIMWI na UKIMWI upo ni wajibu wa kila Mwananchi kuendelea kuchukua tahadhari,” alibainisha

Aidha kauli mbiu yetu inyosema; JAMII IONGOZE KUTOKOMZEA UKIMWI inatuhamasisha jamii yenyewe ndio iongoze mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI

Akizungumzia kuhusu malezi, ametoa rai kwa wazazi kukaa na familia na kuwaelimisha uwepo wa tatizo hili la UKIMWI.

“Tunajukumu kubwa la kuendelea kutoa malezi bora kwa watoto wetu na kuwajengea misingi ya tabia njema” alifafanua

Awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema maandalizi kuelekea wiki Maadhimisho ya siku ya UKIMWI yanaendelea vizuri

“Lengo ni kupeleka ujumbe kwa wananchi, huku tukitupia jicho kwa kundi la vijana na kwa kushiriki kwao itasaidia kupeleka ujumbe kwa vijana wengine ambao hawakupata fursa ya kushiriki,” alisema