Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

“Tuzo ya ushindi Sabasaba iwe nguzo ya kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi” Dkt. Yonazi


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Ofisi yake kwa kundi la watoa huduma bora  na banda bora ngazi ya za Wizara zilizoshiriki katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es salaam iwe nguzo ya Kutoa huduma bora na kwa upana  zaidi kwa wananchi.

Ameyasema hayo mapema leo tarehe 17 Julai, 2024 baada ya kupokea Tuzo hiyo Ofisini kwake Jijini Dodoma ambapo Dkt. Yonazi alitoa shukrani kwa viongozi wa Ofisi hiyo na Taasisi zake kwa maandalizi mazuri na kuongeza kusema kuwa, tuzo hiyo pia itawezesha  Ofisi kufikia malengo ya Serikali na Maono ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuleta tija kwa Taifa.

“Naamini Mwakani tunaweza kufanya vizuri zaidi kwa kuchukua ushindi wa jumla na siyo katika hutoaji huduma bora na banda bora, hivyo hii iwe kama changu ya kuamsha morali kwa watumishi wote wa Ofisi ya Waziri Mkuu.” Alisisitiza Dkt YonaziKwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Anderson Mutatembwa alitoa pongezi kwa timu nzima iliyoshikiri katika maandalizi hayo na kusema hii na dalili nzuri inayoonesha utekelezaji wa maagizo na miongozo inayotolewa na viongozi wa ngazi za juu.

Awali, akiongea wakati wa kaukabidhi Tuzo Hiyo Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Maandalizi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Condrad Millinga alisema kupitia maonesho hayo wananchi waliofika katika banda hilo walipata nafasi ya kufahamu majukumu yanayotekelezwa na Ofisi pamoja na Taasisi zake.

“Wanachi walipata elimu kuhusu namna tunavyotekeleza majukumu ya Ofisi pamoja na kuwahudumia kwa ubora, hii ilichangia kuongeza tija ya uwepo wa banda la Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake katika maonesho hayo,” Alieleza Millinga

 

=MWISHO=