Habari
NEC Yaanza maandalizi ya Uchaguzi Mkuu 2025
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa kuzingatia utaratibu na vigezo.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga wakati akijibu maswali ya baadhi ya wabunge walioomba majimbo yao yagawanywe.
Amesema muda utakapofika, Tume itatoa tangazo rasmi kwa wadau wote wa uchaguzi juu ya kuanza kwa machakato wa ugawaji wa majimbo ili wadau wawasilishe maoni na maombi yao na hivyo kushughulikiwa kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa kikatiba.
Mhe. Ummy amesema majimbo mengi yameomba kugawanywa lakini mambo yanayotazamwa ni pamoja na ukubwa wa ukumbi wa jimbo, idadi ya wabunge wa viti maalumu na jiongrafia za maeneo yaliyoomba kugawanywa.