Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Naibu Waziri Mkuu ashiriki sherehe za miaka 60 ya JWTZ


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameshiriki katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyofanyika leo Septemba 1, 2024 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. 

Maadhimisho hayo yameongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Kuhudhuriwa na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philipo Mpango, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa.

=MWISHO=