Habari
Mwili wa Marehemu Mhe. Lukuvi ukiwasili katika  Kiwanja cha Ndege cha Iringa
Mwili wa aliekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), na Mbunge wa Jimbo la Isimani, Mhe. William Lukuvi, ukiwasili katika Kiwanja cha Ndege cha Iringa tarehe 29 Machi, 2026.
Mwili huo umesafirishwa kutoka Dar es Salaam leo baada ya shughuli ya kuaga iliyofanyika jana Machi 28, 2026 katika Viwanja vya Karimjee.




